Fursa
Umeshawahi kusikia kozi inaitwa Bachelor in Optometry?
Bachelor in Optometry ni shahada ya kwanza inayomfundisha mwanafunzi kila kitu kinachohusu macho, kuona na teknolojia ya ukaguzi pamoja na matibabu ya matatizo ya macho. Hii ni taaluma muhimu sana, kwani matatizo ya macho yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kutokana na mabadiliko ya maisha ya kisasa, matumizi ya muda mrefu kwenye kompyuta na simu, pamoja na magonjwa ya macho yanayoletwa na umri.
Optometry ni taaluma inayohusu upimaji wa macho, utambuzi na tiba ya matatizo ya kuona. Wataalamu hawa huitwa Optometrists, na wanasaidia wagonjwa wenye matatizo ya kuona kama myopia (kuona kwa karibu tu), hypermetropia (kuona mbali tu), astigmatism, presbyopia na matatizo mengine ya macho. Pia, wanahusika na kushauri na kuandaa miwani na contact lenses, na mara nyingine kushirikiana na madaktari wa macho (ophthalmologists) katika upasuaji wa macho kama vile laser eye surgery.
Katika kozi ya Bachelor in Optometry, mwanafunzi hujifunza masomo muhimu yanayohusiana na afya ya macho. Haya ni pamoja na Anatomy na Physiology ya jicho, ili kuelewa mfumo wa macho unavyofanya kazi; Optics, kuhusu jinsi mwanga unavyoingia machoni na namna ya kurekebisha matatizo ya kuona; na Clinical Optometry, inayohusisha mbinu za kupima macho kitaalamu. Vilevile, wanafunzi hufundishwa kutumia Ophthalmic Instruments za kisasa kwa ajili ya upimaji wa macho, kushughulika na Contact Lenses & Low Vision Aids kusaidia wenye uoni hafifu, na pia kujifunza kuhusu Ocular Diseases, magonjwa ya macho na mbinu za kuyatibu.
Fursa za ajira kwa mhitimu wa Optometry ni nyingi na pana. Wanaweza kufanya kazi katika hospitali kubwa za macho kama CCBRT, Muhimbili, Aga Khan na KCMC, au kwenye clinics binafsi za macho. Aidha, mhitimu anaweza kuanzisha au kufanya kazi katika optical shops zinazouza miwani na kutoa huduma za kupima macho. Kwa wale wanaopenda taaluma ya utafiti na elimu, kuna nafasi katika vyuo vikuu na taasisi za utafiti wa macho. Pia, mashirika ya afya ya macho ya kimataifa kama Sightsavers, Fred Hollows Foundation na Vision 2020 huwapa nafasi kubwa ya ajira Optometrists.
Kwa upande wa kujiajiri, mhitimu wa Optometry anaweza kufungua optical shop au clinic ndogo ya macho, kutoa huduma za mobile eye clinic hasa vijijini ambako upatikanaji wa huduma hizi ni mdogo, au hata kuanzisha biashara ya miwani na lensi.
Kwa sasa, Tanzania ina Diploma ya Optometry pekee, na bado hakuna shahada ya kwanza. Hii ina maana kwamba wanaosoma Bachelor in Optometry nje ya nchi, hususan India, wanapokuwa wamemaliza masomo hupata nafasi kubwa zaidi ya ajira, nafasi za uongozi katika mashirika na hospitali za macho, na hata heshima ya kitaalamu zaidi katika soko la ajira.
Kozi hii ni ya maana sana kwa sababu wagonjwa wa macho nchini Tanzania na Afrika Mashariki ni wengi sana huku wataalamu wakiwa wachache. Pia, ni taaluma inayochanganya afya na biashara, kwa kuwa mhitimu anaweza kuwa mtaalamu wa macho na wakati huohuo kuwa mfanyabiashara wa opticals. Kwa kuwa hakuna shahada ya Optometry nchini Tanzania, mhitimu wa ngazi hii anakuwa na faida kubwa kwenye soko la ajira.
Kupitia Akili Education, mwanafunzi anaweza kupata nafasi ya kusomea Bachelor in Optometry katika vyuo bora nchini India vinavyotambulika kimataifa, kwa gharama nafuu ya takribani milioni 8 tu kwa mwaka ikijumuisha ada, malazi na chakula. Hii ni fursa bora kwa vijana na wazazi wanaotaka kuwekeza katika taaluma yenye heshima, ajira ya uhakika, na upeo mkubwa wa kitaifa na kimataifa.
Frequently Asked Questions
Have questions about studying abroad or working with Akili Education? You’re not alone — here are some of the most common questions students and parents ask us. If you don’t find what you’re looking for, our team is always here to help.
What Bachelor degree courses do you advice a form 6 CBG graduate to study?
We advice a CBG form six graduate to study the following courses which are on high demand; Bachelor in Biotechnology, Bachelor in Microbiology, Bachelor in Forensic Sciences, Bachelor in Information and Technology etc
What Engineering courses are on demand right now?
Engineering courses that are on demand right now include Computer Science and Engineering programs with specialisations like, Cyber Security, Artificial Intelligence, Data Science, Blockchain Technology.
Which country gives quality and affordable education comparing to Tanzania Standard of Living?
The answer to this question has always been India. India has top ranked universities giving Bachelor and Masters degree program for a budget of 8 million Tanzania Shillings per year, which includes tuition fee, hostel and food per year.
Apart from Medicine, what other courses can a PCB form 6 graduate study for his/ her bachelor degree?
PCB graduate can pursue the following programs for their bachelor degree: Bachelor in Radiology, Bachelor in Optometry, Bachelor in Medical Laboratory Technology, Bachelor in Physiotherapy, Bachelor in Cardiovascular technology, Bachelor in Anaesthesia Technology, Bachelor in Dialysis Technology, Bachelor in Operation Theatre Technology
What countries can Akili Education help me pursue my study abroad dreams?
Depending on your budget, Akili Education can help you secure admission into top ranked universities around the world in countries like UAE, UK, USA, Canada, Spain, India, Mauritius, Malaysia and many others
